Thursday 27 February 2014

TANGAZO LA KAZI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji.
A.      MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)
         
  • SIFA ZINAZOHITAJIKA
  • Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa  na Serikali katika fani zifuatazo:
Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.
  • Awe na umri usiozidi miaka 35

  • MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
  • Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini
  • Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka
  • Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji
  •     Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali
  • Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji
  •  Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia na Kutoka Nchini
  • Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili
  • Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini
  • Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia
  • Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa

B:      KOPLO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)      
1.      SIFA ZINAZOHITAJIKA:
  • Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
  • Awe na umri usiozidi miaka 30
C.      KONSTEBO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)
1.      SIFA ZINAZOHITAJIKA:
  • Awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu
  • Awe na umri usiozidi miaka 25
D:      SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI
  • Cheti cha Ufundi Stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya Umeme na Mitambo
  • Cheti au Stashahada ya Uhaziri (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu (Certificate in Records Management) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statatistics ) Kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Cheti au Stashahada ya Vyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operations) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada katika fani ya Uchapaji (Printing)
  • Ujuzi na Elimu ya Kompyuta na Uandishi mzuri utazingatiwa
  • Cheti cha Ufundi Makanika,Kozi ya juu ya Udereva na Leseni ya Udereva Daraja C

E.       MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
  •  Kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji
  •      Kuandika Hati mbalimbali za Uhamiaji
  • Kufanya doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
  • Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini
  • Kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara.
  • Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji.
  • Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji
  • Kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji
F.       MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATISHO VIFUATAVYO:
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo kwa mujibu wa sifa zilizotajwa
  • Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
  • Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  • Picha mbili (Passport Size)
  • Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
G.      UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapitie posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.
  • Maombi ya nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji yatumwe kwa:

KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P. 9223,
DAR ES SALAAM
  • Maombi ya nafasi ya Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji yatumwe kwa:

KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P. 512,
DAR ES SALAAM
         
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi zote ni tarehe 27/02/2014

VACANCY ANNOUNCEMENT
The Principal Commissioner of Immigration Services announces vacant Posts in the Immigration Department.  Any Tanzanian Citizen with minimum qualifications mentioned hereunder is encouraged to apply:
A.      ASSISTANT INSPECTOR OF IMMIGRATION SERVICES (70 Posts)
  • Qualifications:
    • Tanzania Citizens aged not above 35 years
    • Holder of Bachelor Degree or Advanced Diploma from any University or Institution recognized by the Tanzania Government in the following disciplines:

Law, Economics, Business, Administration, Journalism, Education, Transportation, Human Resource, Computer Science, Information and Communication Technology, Statistics, Printing, Civil Engineering and Mechanical Engineering
  • Duties and Responsibilities:
  • To supervise patrols along the border areas, sea ports, bus stands, highways, railway stations, business centres and other entry points
  • To prepare charge sheets and prosecute in court all immigration related cases
  • To issue and receive various application forms for immigration services
  • To execute preliminary scrutinization of different application forms
  • To authorize opening of customers application files
  • To receive and scrutinize Passports and other travel documents
  • To authorise collection of government revenues for various immigration services
  • To keep records of all persons entering or leaving the country
  • To collect, organize and keep statistics of immigration and citizenship services
  • To notify customers in writing on the status of their applications

B.      CORPORAL OF IMMIGRATION SERVICES (100 Posts)
  • Qualifications:
    • Tanzania Citizens not above 30 years of age
    • Holder of Advanced Certificate of Secondary Education

C.      CONSTABLE OF IMMIGRATION SERVICES (100 Posts)
  • Qualifications:
    • Tanzania Citizens not above 25 years of age
    • Holder of Certificate of Secondary Education

D.      ADDED ADVANTAGES:
  • Certificate or Diploma in Law
  • Computer knowledge and typing
  • Full Technician Certificate (FTC) in Electricity and Mechanical Engineering
  • Certificate or Diploma in Secretarial duties
  • Certificate or Diploma in Records Management
  • Certificate or Diploma in Statistics
  • Certificate or Diploma in Marine Transport and Operations
  • Certificate in Trade Test Grade II, Advanced Drivers Course Grade II and Driving License Class C
  • Certificate or Diploma in Printing
  • Certificate or Diploma in Civil Engineering
  • Certificate or Diploma in Statistics
  • Duties and Responsibilities:

  • To conduct patrols along the border areas, sea ports, bus stands, highways, railway stations, business centres and other entry points
  • To conduct inspections in the hotels, guest houses and other business premises
  • To issue Immigration forms and information on the requirements for the services sought 
  • To escort immigration accused aliens/citizens in court
  • To escort deported aliens outside the country
  • To open and keep customers’ files in good order
  • To apprehend suspected immigration offenders
  • To make maintenance and regular service of equipment
  •   To collect, organize and keep immigration related statistics
NOTE: Selected applicants for the posts must attend a one year Basic Immigration Course prior to employment
D.      APPLICATION LETTERS MUST BE ACCOMPANIED WITH:
  • Two recent passport size photographs
  • Photocopy of Academic Certificates/Trainings
  • Photocopy of Birth Certificate
  • Letter of Introduction from Village/Ward Executive Officer or Sheha
  • Secondary/Advanced Secondary School Leaving Certificate
  • Primary school leaving Certificate
E.       MODE OF SUBMISSION
          All applications must be hand written and have to be submitted through Post Office
  • All applications for the post of Assistant Inspector of Immigration Services should be channeled to:

The Permanent Secretary,
Ministry of Home Affairs,
P.O. Box 9223,
DAR ES SALAAM
  • All applications for the post of Corporal and Constable of Immigration Services should be channeled to:

The Principal Commissioner of Immigration Services,
P.O. Box 512,
DAR ES SALAAM
Deadline for submission of applications: February 27, 2014.

Tuesday 11 February 2014

MBIO ZA URAISI 2015 KUVURUGA BUNGE LA KATIBA

BAADHI ya wagombea wanaotajwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wanadaiwa kuanza kujenga makundi ya kupinga serikali tatu ndani ya Bunge la Katiba, imefahamika.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili limezipata, wanasiasa hao wanaamini kwamba chini ya mfumo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Tanzania hatakuwa na nguvu kama alizonazo sasa Rais Jakaya Kikwete.
Raia Mwema limeambiwa kwamba wagombea hao wameandaa makundi ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kushawishi wajumbe wa Bunge hilo wasikubali muundo wa serikali tatu.
“Tunachotaka sisi ni serikali mbili kama ilivyo sasa, zikiwa na mabadiliko kidogo kwa ajili ya Zanzibar. Watu wanataka urais kwa sababu wanataka wawe na mamlaka ambayo anayo Kikwete sasa.
“Kuna faida gani kuwa Rais wa Tanganyika wakati si Amiri Jeshi Mkuu? Kuna faida gani ya kuwa Rais wa Tanzania wakati rasilimali zote muhimu ziko kwa nchi washirika?
“Huyu rais wa Tanzania atageuka kuwa ombaomba na siku marais wenzake washirika wakiamua kumuwekea ‘kauzibe’ basi atabaki amekaa Ikulu bila lolote la maana.
“Utaona kwenye Bunge la Katiba. Sisi tutapambana kuhakikisha kwamba suala la serikali tatu linashindwa. Ni ama serikali mbili zilizoboreshwa au hakuna serikali tatu,” alisema mmoja wa wapambe wa mmoja wa wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kutaka kuwania urais.
Gazeti hili limeambiwa kwamba kampeni hizi dhidi ya serikali tatu ndani ya Bunge hilo zitapamba moto na kuwa hadharani mara baada ya kutangazwa kwa majina ya wajumbe wa Bunge hilo wakati wowote kutoka sasa.
Raia Mwema limeambiwa kwamba wenye nia hiyo wanajua kwamba watahitaji kura zisizozidi 310 ndani ya Bunge hilo, kuhakikisha kwamba suala hilo halipitishwi.
Rais Kikwete tayari ametangaza kwamba endapo Rasimu ya Katiba haitapitishwa katika Bunge hilo, Tanzania itaendelea kutumia iliyopo; jambo ambalo litapokewa kwa furaha na wagombea hao.
Akizungumzia hali hiyo, mmoja wa wajumbe wa Tume ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, aliliambia gazeti hili wiki hii kwamba wao hawakufanya kazi kwa kuangalia wanaotaka urais wanahitaji nini, bali maslahi ya wananchi.
“Kilichopendekezwa na Tume kimetokana na maoni ya Watanzania walio wengi. Kama kuna watu wanafikiri vingine, sisi hatujui kwanini lakini tulitakiwa kukusanya maoni ya wananchi na kilichopo kwenye ripoti ndicho wanachotaka,” alisema Baregu.

SOURCE;  http://www.raiamwema.co.tz TOLEO 336

“Kilichopendekezwa na Tume kimetokana na maoni ya Watanzania walio wengi. Kama kuna watu wanafikiri vingine, sisi hatujui kwanini lakini tulitakiwa kukusanya maoni ya wananchi na kilichopo kwenye ripoti ndicho wanachotaka,” alisema Baregu
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/urais-kuvuruga-bunge-la-katiba#sthash.EmT1b13D.dpuf

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/urais-kuvuruga-bunge-la-katiba#sthash.Vew4Qhnr.dpuf

Tuesday 4 February 2014

NGONO YA MDOMO NI HATARI

Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,
 pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa  ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747  na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni  kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki ngono.
Vijana  wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni  ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa na ile ya  ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze  kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema  Dk Kahesa na kuongeza. Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi  kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani  nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema  katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo  inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea  hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza  ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa  bado wadogo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata  watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea  kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati  bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni “Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote  hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema  kuharibu seli ambazo zipo katika  utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika  maeneo mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa kula vyakula vyenye  asidi, vyakula  vichachu, vyakula vyenye pilipili, pombe kali na  vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha saratani.
Anasema  asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road wanakuwa na  historia ya kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.

Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za  mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona  viashiria kwani mwanzo  mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa  kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
“Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri  siku zinavyokwenda  ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo  na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja,” anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama  saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo  vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi  au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa  kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa,  wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu  wenye  umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri

Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa  gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria  na kwamba ugonjwa huu pia  huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
Hepatitis A: Hiki ni  ni kirusi kinachopatikana  katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C:  ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa uchache lakini  kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa katika mdomo  wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema  hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
“Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam domo”anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake  na kwamba staili hizo  ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya  utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina  madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii  kina  manufaa la hashaa!  vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.